
Inasikitisha sana kuona kesi nyingi za watoto kuhusu ubakaji, utesaji, utelekezaji, kuchomwa moto, kufungiwa ndani na matukio mengine mabaya kama hayo yanachukua muda mrefu baada ya kufika mahakamani na aghalab washtakiwa huonekana katika jamii wakiendelea na shughuli zao kama kawaida huku watoto wakiwa tayari wameathirika kisaikolojia.
Kumekuwepo malalamiko ya kesi za ukatili wa watoto kuchukua muda mrefu mahakamani kwa visingizio kuwa upelelezi haujakamilika ama mashahidi hawatoshelezi, hali inayolaumiwa sana na jamii na kuwakatisha wengi tama ya kuripoti kesi hizo kwani wengi wanaona ni kupoteza muda bure.