Maradhi yanayosababishwa na vyakula ambavyo havijatayarishwa vizuri yanapelekea idadi ya watu million 81 kupata maradhi kila mwaka, na takriban watu 9000 wanapoteza maisha kutokana na maradhi haya. Watoto wapo hatarini zaidi kupata maradhi kutokana na chakula kibovu.
Kumlinda mtoto wako dhidi ya bacteria ambao wanasababisha kuharibika kwa chakula,ni muhimu kutumia njia salama za kuhifadhi chakula, ikiwemo kumuepusha na chakula kilichokuwa hakijapikwa vizuri au kisichohifadhiwa kwenye friji kama vile nyama,samaki au mayai. Safisha mikono yako,vyombo vya mtoto pia kosha matunda vizuri. Usimpe mtoto maziwa ambayo hayajachemshwa na juice na chemicals.Usimpe mtoto chakula kilichokaa sana kwenye fridge na kwenye joto vitampelekea kuharisha na kupoteza kinga mwilini. |