Kitaalamu, wakati wote ni wa mazoezi ikiwemo wakati wa ujauzito, ambapo yanaweza kufanya maajabu.
Kwanza, mazoezi huongeza hisia za mwili wa mama, humsaidia mama kupata usingizi na hupunguza maumivu ya mgongo.
Pia, mazoezi kwa mama mjamzito humuandaa mama na kumpa nguvu wakati wa kujifungua.
Mjamzito anapofanya mazoezi, hutanua misuli ya kiuno na ile ya njia ya uzazi. Mazoezi huipa nguvu na uvumilivu misuli wakati wa kujifungua.
Misuli inapokuwa mwepesi, huwa ni rahisi mwili huo kurudi katika umbile lake la awali mapema mara baada ya kujifungua.
Mjamzito anapofanya mazoezi, huufanya moyo wake kupata mapigo mazuri na kupelekea mzunguko mzuri wa damu.
Mazoezi humfanya pia mama mjamzito asiongezeke uzito na kumuepusha na pressure.
Mazoezi haya huepusha wingi wa mafuta mwilini, na kuzuia maradhi ya mishipa ya damu kwa mjamzito.
Mzunguko mzuri wa damu huepusha damu kuganda tendo linalosababisha kukwama kwa usambazaji wa damu mwilini, (moyo, ubongo na mapafu).
Mazoezi yafuatayo ni mazuri kwa mama anayetarajia kupata mtoto. Ingawa baadhi ya mazoezi yanaweza yasiwe na matokeo mazuri kwa mama ambaye amebakiza siku chache za kujifungua.
Hata hivyo, mama anatakiwa kuhakikisha anawasiliana na daktari wake kabla hajafanya uamuzi wa aina ya mazoezi ya kufanya.